Jafo: Bahari ni nyenzo ya kujenga uchumi

0
141

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amesema, bahari ni nyenzo muhimu katika kujenga uchumi wa nchi na kuinua kipato cha wananchi wanaofanya shuguli za uvuvi.

Waziri Jafo ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam mara baada ya ufunguzi wa washa ya kikanda ya Umoja wa Mataifa kuhusu usimamizi wa mazingira ya bahari.

Amesema warsha hiyo itakuwa msaada katika kuzisadia jamii zinazozungukwa na bahari kutambua fursa za kiuchumi na hatimaye kujiongezea kipato.

Pia ameeleza kuwa kupitia warsha hiyo changamoto mbalimbali za mabadiliko ya Tabianchi zitajadiliwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi kutoka Zanzibar Dkt. Aboud Suleiman Jumbe amesema, warsha hiyo itakuwa chachu katika upatikanaji wa taarifa sahihi za kimazingira, shuguli za uvuvi zinazofanyika baharini na itachochea maendeleo ya watu.

Zaidi ya washiriki hamsini kutoka ndani na nje ya nchi wanashiriki warsha hiyo, ambapo kwa Tanznaia ni mara ya pili kufanyika.

Warsha hiyo inaratibiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Waziri Jafo ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam mara baada ya ufunguzi wa washa ya kikanda ya Umoja wa Mataifa kuhusu usimamizi wa mazingira ya bahari.

Amesema warsha hiyo itakuwa msaada katika kuzisadia jamii zinazozungukwa na bahari kutambua fursa za kiuchumi na hatimaye kujiongezea kipato.

Pia ameeleza kuwa kupitia warsha hiyo changamoto mbalimbali za mabadiliko ya Tabianchi zitajadiliwa.

Zaidi ya washiriki hamsini kutoka ndani na nje ya nchi wanashiriki warsha hiyo, ambapo kwa Tanznaia ni mara ya pili kufanyika.

Warsha hiyo inaratibiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi kutoka Zanzibar Dkt. Aboud Suleiman Jumbe amesema Mkutano huo utakuwa chachu katika upatikanaji wa taarifa sahihi za kimazingira,shuguli za uvuvi zinazofanyika baharini ili ziweze kusimamiwa ipasavyo nakuchochea maendeleo ya watu.