Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amezipa wiki moja Hamashauri zote nchini kuwasilisha taarifa ofisini kwake kuhusiana na mikopo yoyote waliyoichukua kutoka katika taasisi za fedha.
Jafo amezitaka halmashauri hizo kueleza aina ya mikopo hiyo na riba zake.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kuzitaka Halmashauri zote nchini kuacha kukopa katika mabenki.
Aidha amezitaka halmashauri ambazo zimekopa na bado hazijaitumia mikopo hiyo kuirejesha mara moja.
Jafo pia amemuagiza Katibu Mkuu wa TAMISEMI kuhakikisha anawasimamia Wakurugenzi na makatibu Tawala wote.
@ortamisemi