JAFO AWATAKA VIONGOZI KUSIMAMIA ZOEZI LA KUWARUDISHA WANAFUNZI NYUMBANI

0
204

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo ametoa agizo kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa shule kote nchini kusimamia zoezi la kuwasafirisha wanafunzi kurudi nyumbani kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa CORONA.

AWaziri JAFO ametoa agizo hilo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari, kufuatia agizo lililotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kufungwa kwa shule za Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo Vikuu kabla ya tarehe 20 mwezi huu kuepuka maambukizi ya ugonjwa wa CORONA.