Isaya Mwita apewa siku 14 kukabidhi ofisi ya Meya wa Dar es Salaam

0
159

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana amempa Isaya Mwita siku 14 kuanzia Januari 10 kukabidh ofisi ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kuvuliwa wadhifa hao na kikao cha Madiwani wa Halamshauri ya jiji hilo.

Januari 9 mwaka huu kikao maalumu cha Baraza la Madiwani la jiji hilo kilikutana kwa ajenda moja ya kupokea ripoti ya tuhuma dhidi ya Meya Mwita kisha kupiga kura ya kutokuwa na imani naye huku kura zilizoonesha kutokuwa na imani naye zikiwa 16.

Mwita ambaye ni Diwani wa Vijibweni amesisitiza kuwa bado yeye ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam kwa maelezo kuwa mchakato wa kumuondoa madarakani haukufuata sheria kwa theluthi mbili (wajumbe 17) inayotakiwa ili aondolewe haikufikiwa, na kwamba anataka arejeshewe gari la ofisi yake lililochukuliwa.