Ireland kuipatia Tanzania bilioni 3.8

0
233



Ireland imeahidi kuipatia Tanzania msaada wa Euro Milioni 1.5 ( shiliongi bilioni 3.8) ambazo zitatumika katika shughuli mbalimbali.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi mara baada ya kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa na Masuala ya Diaspora wa Ireland, Ciaran Cannon, mazungumzo yaliyofanyika kwa njia ya video.

Wakati wa mazungumzo hayo, Waziri Kabudi ameiomba Ireland iisaidie Tanzania kuiomba jumuiya ya kimataifa kuifutia madeni yake ili iweze kutumia fedha hizo katika mapambano dhidi ya corona.