IMF kusaidia masuala ya kijinsia

0
150

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania inaunga mkono mpango ulioanzishwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) la kuingiza masuala ya kijinsia kwenye utekelezaji wa mipango yake ya maendeleo.

Dkt. Nchemba ametoa kauli hiyo mkoani Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa majadiliano kuhusu mkakati wa IMF wa kuingiza masuala ya kijinsia kwenye mipango yake.

Amesema serikali itaendelea kutilia mkazo masuala hayo ya kijinsia kwa kuwekeza rasilimali fedha katika kuboresha afya ya mama na mtoto, utoaji elimu bila ada na kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kufanikisha masuala hayo.

Mkutano huo wa majadiliano kuhusu mkakati wa IMF wa kuingiza masuala ya kijinsia katika mipango yake, umehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.