IGP Sirro Mwenyekiti mpya EAPCCO

0
180

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro, leo amekabidhiwa rasmi Uenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa afrika (EAPCCO) kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Sudan, -Adil Mohamed Ahmed.

Tukio hilo limeshuhudiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, -Mrisho Gambo pamoja na Wakuu wa vyombo mbalimbali vya Ulinzi na Usalama hapa nchini.

Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha ( AICC), ambako kunafanyika mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika.