IGP Sirro: Hatutoruhusu mtu kuvuruga amani kwa maslahi binafsi

0
253

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro ameonya kwamba Jeshi la Polisi halitoruhusu watu wachache wavuruge amani ya nchi kwa maslahi yao binfasi.

Ametoa kauli hiyo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani leo Novemba 23 Arusha.

Ameeleeza kwamba matukio ya kihalifu yamepungua nchini, lakini bado zipo changamoto mbalimbali ikiwemo tishio la vitendo vya kigaidi, ambavyo jeshi hilo linaendelea kupambana navyo.

Kuhusu usalama barabarani IGP amesema kwa makosa ya barabarani yamepungua kwa asilimia 15.4 tangu Januari mwaka huu, jambo linaloonesha matokeo chanya katika jitihada za kutoa elimu.

Akitoa taarifa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilboard Mutafungwa amesema tangu Januari hadi Setemba 2021 madereva 537 wamefungiwa leseni zao kwa makosa ya barabarani huku zaidi ya 100,000 wakitozwa faini na wengine kupewa onyo kali.

Ametoa ombi kwa Rais Samia la kuweza kufungwa kamera za ulinzi kwenye barabara za miji na barabaara kuu ili kupunguza ajali kwa kulazimisha madereva kufuata sheria, kanuni na miongozo ya kutumia barabara.

Aidha, amesema kamera hizo zitaongeza uwazi katika utendaji wa jeshi na wananchi, zitapunguza idadi ya askari barabarani na kuharakisha upelelezi wa matukio ya barabarani.

Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa mwaka 2021 itakayoisha Novemba 28 ikiwa na kaulimbiu isemayo ‘Jali Maisha Yako na ya Wengine Barabarani.’