Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro, amewataka vijana wanaoendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, kufuata sheria na alama za barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
IGP Sirro ameyasema hayo akiwa Kiwangwa mkoani Pwani wakati akizungumza na baadhi ya madereva wa bodaboda pamoja na wakazi wa eneo hilo wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Tanga.
Amesema karibu asilimia 90 ya vifo vinavyotokea hapa nchini vinatokana na ajali za pikipiki, hivyo ni vema madereva wa vyombo hivyo wakaongeza umakini wawapo barabarani.
Pia amewataka kutojihusisha na vitendo vya uhalifu ili usafiri huo uendelèe kuaminiwa na watumiaji wengi.