IGP Sirro awanyooshea kidole wanaofanya ujambazi

0
226

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amewataka watu wote wanaojihusisha na vitendo vya ujambazi kuacha mara moja kwani Jeshi lake limejipanga kuhakikisha linakabiliana na matukio hayo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa majengo ya Chuo cha Taaluma cha Polisi mkoani Dar es Salaam, IGP Sirro amesema jeshi hilo linaendelea na oparesheni mbalimbali na kuhakikisha linatokomeza kabisa vitendo vya uhalifu kwa kutumia silaha hapa nchini.

IGP Sirro amewataka watu wanaoendeleza vitendo vya uhalifu kuacha mara moja kwani Watanzania wanataka kufanya shughuli zao kwa amani na kwamba jeshi hilo halitawafumbia macho wahalifu.

“Mama mtunze mwanao, mwanamke mtu mumeo, usipowatunza utawakosa,” ameeleza IGP Sirro katika msisitizo wake kuhusu kukabiliana na uhalifu.

Akizungumzia kuhusiana na oparesheni za kukagua magari yanayotozwa faini na kukaidi kulipa madeni yao, IGP Sirro amewataka wamiliki wa vyombo vya moto kulipa madeni yao na kuacha kujificha kwani fedha hizo ndizo zinazotumika kununua dawa.

Amezungumzia pia namna Jeshi la polisi linavyokabiliana na makossa ya barabarani ambayo amesema pia yanapungua kwa kiasi kikubwa kutokana na udhibiti unaofanywa na kikosi cha usalama barabarani.