IGP Sirro atembelea hospitali Kuu ya Jeshi la Polisi

0
394

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali Kuu ya Jeshi hilo iliyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam na kujionea namna hospitali hiyo inavyotoa huduma za matibabu kwa wananchi wanaofika hospitalini hapo.

Akizungumza na uongozi wa hospitali hiyo IGP Sirro amewataka Waganga na Wauguzi kufanyakazi za kitabibu kulingana na viapo vyao,  huku wakihakikisha wanatoa huduma bora za matibabu kwa wateja.

Akiwa katika hospitali hiyo, IGP Sirro pia amekagua jengo la kuhifadhi maiti,  ambalo ujenzi wake unakaribia kukamilika.

Wakati  huohuo IGP Sirro amekagua ukarabati wa Chuo cha Maofisa wa Polisi kilichopo Kurasini jijini Dar es salaam, ukarabati unaofanyika baada ya Rais John Magufuli kutoa Shilingi Milioni 700  kwa ajili ya ukarabati huo.