IGP Sirro asisitiza kudumishwa kwa amani

0
159

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro amewataka Wadau wa amani na Viongozi wa dini nchini kuhubiri amani pamoja na kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili katika jamii ikiwa ni pamoja na udhalilishaji na matumizi ya dawa za kulevya.

IGP Sirro ametoa wito huo kisiwani Zanzibar, akiwa katika ziara yake ya kikazi.

Amewataka Watanzania wote kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha nchi inakua salama.