IGP apangua baadhi ya makamanda

0
142

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Camillus Wambura, amewabadilisha vituo vya kazi baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa na mmoja kumuhamishia Makao Makuu ya polisi Dodoma.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime imeeleza kuwa, katika mabadiliko hayo Henry Mwaibambe aliyekuwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita amehamishiwa mkoa wa Tanga kuwa kamanda wa polisi wa mkoa huo.

Aliyekuwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga, Safia Shomary yeye amehamishiwa mkoa wa Geita kuwa kamanda wa polisi wa mkoa huo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, aliyekuwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Richard Ngole amehamishiwa Makao Makuu ya polisi Dodoma, huku nafasi yake ikichukuliwa Kungu Malulu ambaye alikuwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Kipolisi wa Rufiji.