Idris Sultan na wenzake wawili wafutiwa kesi mahakamani

Kisutu Dar es salaam

0
144

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam imewafutia kesi nakuwaachia huru mchekeshaji Idris Sultan na wenzake wawili.

Uamuzi huo umetolewa hii leo mbele ya hakimu mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Yusto Ruboroga baada ya upande wa Mashtaka kuwasilisha hati kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP ikieleza kuwa DPP hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washitakiwa hao.

Katika kesi ya Msingi washitakiwa wanadaiwa kuchapisha maudhui kwenye mtandao bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.

Idris na wenzake wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 8, 2016 na Machi 13, 2020 katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na Dokta Ulimwengu na Isihaka Mwinyimvua ambao wote ni wakazi wa Dar es Salaam.