Idadi ya watalii yaongezeka kwa asilimia 44

0
118

Katika kipindi cha Januari hadi Mei, 2022 idadi ya watalii waliotembelea Tanzania ilifikia 458,048, sawa na ongezeko la asilimia 44.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka 2021 ambapo walipokelewa watalii 317,270.

Takwimu hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja wakati wa mapokezi ya watalii 60 kutoka nchini Marekani jijini Dar es Salaam.

“Marekani ni miongoni mwa masoko yetu ya utalii ya kimkakati yaliyoanza kuonesha matumaini makubwa katika kuirejesha Sekta ya Utalii baada ya kuathirika na Janga la UVIKO-19, kwa mfano mwaka 2021 tulipokea watalii 48,537 kutoka nchini humo sawa na ongezeko la asilimia 55 ikilinganishwa na watalii 31,211 kwa mwaka 2020” amefafanua Masanja.

Aidha, ameweka bayana kuwa ongezeko hilo la idadi ya watalii ni kutokana na programu maalumu ya kimkakati ya Tanzania:The Royal Tour iliyoasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan,