Taaasisi ya utafiti wa wanyamapori Tanzania TAWIRI imesema katika baadhi ya tafiti walizofanya hapa nchini imebaini kuongezeka kwa Idadi ya wananyapori kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Akizungumza na TBC Dr Wilfred Marealle ambaye ni mtafiti kutoka TAWIRI amesema udhibiti wa hifadhi za mazingira kwa kushirikiana na serikali pamoja na wanannchi umechangia kuleta mabadiliko
Hayo
Kwa upande wake mtafiti kutoka TAWIRI Dr Jerome Kimara amesema tafiti wananzofanya zinawafikia mamlaka husika ili kuchukua hatua mbalimbali na mwaka huu watakuwa na kongamano la kuwasilisha tafiti n yingine ili ziweze kusaidia Taifa katika kukuza sekta ya utalii nchini