Idadi ya waliokufa kwa Corona yafikia watatu

0
524

Wizara ya Afya nchini Tanzania imetoa taarifa kuhusu wagonjwa wapya watano (5) wenye maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) ambao wote ni Watanzania na ni wakazi wa Dar es Salaam.

Aidha leo Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid ametangaza kuwa na wagonjwa wapya wawili (2) waliothibitika kuwa na Corona hivyo sasa jumla ya watu waliothibitishwa kupata maambukizi ya COVID-19 nchini ni 32.

Kati ya hao, watano (5) wamepona na wagonjwa wengine 24 wanaendelea vizuri na matibabu.

Pia wizara imetoa taarifa ya vifo viwili (2) vilivyotokea leo miongoni mwa wagonjwa waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya COVID-19 na kufanya idadi ya waliokufa kutokana na ugonjwa huu kufikia watatu (3).