Ibada ya kumuombea hayati magufuli

0
804

Ibada maalum ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli imefanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana Maria Muzeyi Parokia ya Mlimani, Chato mkoani Geita na kuongozwa na Askofu Mkuu Jimbo la Katoliki la Rulenge, Ngara, Severine Niwemugizi.

Mjane wa Hayati Magufuli, Janeth Magufuli ameongoza Wanafamilia katika Ibada hiyo ambayo pia imehudhuriwa na viongozi na watu mbalimbali.

Dkt. Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam na kuzikwa Chato mkoani Geita.