Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema kazi iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kubwa hivyo wananchi hawana budi kumuunga mkono kwani ameifungua nchi.
Waziri Nape ameyasema hayo wakati wa Tamasha la Usiku wa Royal Tour lililoandaliwa kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya Utalii hapa nchini.
Amesema tamasha hilo limeandaliwa kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais katika kukuza utalii nchini na kuongeza kuwa matamasha mengine yataendelea kuandaliwa kama muendelezo wa kukuza utalii wa ndani.
“Tumekuja kumuunga mkono Rais Samia, leo tumemleta Koffi, tutaleta na wengine na itakuwa ni bandika bandua” alisema
Waziri Nape amesema mabadiliko chanya katika sekta ya utalii yamezidi kuonekana kupitia idadi ya watalii inayoendela kuongezeka kila siku kutokana na juhudi za Rais Samia kuifungua nchi.