Ikiwa zimesalia siku KUMI kufanyika kwa mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi Zilizo Kusini mwa Afrika – SADC, hapa jijini DSM, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi JOHN KIJAZI ametembelea ukumbi utakapofanyika mkutano huo na kuelezea kuridhishwa na maandalizi
Akiwa katika ukumbi huo wa Mikutano wa Kimataifa wa JULIUS NYERERE, Balozi KIJAZI amesema ni wakati sasa kwa Watanzania kujipanga kuwapokea wageni kwa ukarimu, upendo na kudumisha amani na utulivu wakati wote wa mkutano huo utakaoanza tarehe 9 hadi 18 mwezi Agosti.