Hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi yaahirishwa

0
429

Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa maarufu kama Mahakama ya Mafisadi, imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara Ayubu Kiboko na Mkewe Pilly Mohamed hadi Desemba 18 mwaka huu.

Uamuzi wa kuahirisha kesi hiyo umetolewa na Msajili wa mahakama hiyo David Ngunyale baada ya washtakiwa hao kufikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi yao  iliyotarajiwa kutolewa leo baada ya upande wa mashtaka kufunga jalada la ushahidi lililokuwa na mashahidi 16. 

Katika Kesi ya msingi namba 29/2018, Kiboko na mkewe wanadaiwa kukamatwa Mei 23 mwaka 2018 eneo la Tegeta Nyuki – Masaiti wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam wakiwa wanasafirisha dawa za kuĺevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 251.25 kinyume na sheria.

Hata hivyo sababu za kuahirishwa hukumu ya kesi hiyo hazijatolewa na Mahakama hiyo.