Huduma zasitishwa kanisa lililovamiwa Geita

0
197

Huduma zote za Ki – Ibada na Ki – Sakramenti katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Jimbo Katoliki la Geita zimesitishwa kwa muda kuanzia leo Februari 27, 2023, kufuatia uvamizi na uharibifu wa mali mbalimbali ndani ya kanisa hilo unaodaiwa kufanywa na kijana mmoja.

Taarifa ya kusitishwa huduma hizo imetolewa kwa vyombo vya habari na Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Flavian Kassala.

”Uharifu uliotokea katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Jimbo Katoliki la Geita usiku wa kuamkia Februari 26, 2023 ni kufuru kubwa kwa Sakramenti ya Ekaristi Takatifu na umeivunjia Sakramenti ya Ekaristi Takatifu heshima yake kwa kiasi kikubwa sana” . imesema taarifa ya Askofu Kassala

Amesema uharibifu huo umelinajisi kanisa katika utakatifu wake uliowekwa wakati wa kubarikiwa na kwamba uharibifu uliofanywa umeathiri kwa kiasi kikubwa hadhi ya muumini Mkatoliki na jamii kwa ujumla.