Huduma za kutafsiri nyaraka kuboreshwa

0
145

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega, amewaagiza Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa pamoja Makamishna wa Uhamiaji nchini kuboresha mifumo ya utoaji huduma za kutafsiri nyaraka za wageni wanaotoka nje ya nchi.

Naibu Waziri Ulega ametoa agizo hilo mkoani Dar es salaam, wakati wa ziara yake katika ofisi za Idara ya Uhamiaji zilizopo Kurasini.

Pia ameutaka uongozi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (TATAKI) kuwapa misamiati Wasanii wa kazi za muziki ili waweze kuitumia katika kazi zao za kila siku.