Huduma za afya Kibong’oto zaboreshwa

0
168

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amefungua maabara ya afya ya jamii ya Kibong’oto wilayani Siha, Kilimanjaro.

Akihutubia mara baada ya ufunguzi wa Maabara hiyo, Makamu wa Rais amesema serikali itaendelea kuipa kipaumbele Hospitali ya magonjwa ambukizi ya Kibong’oto kwa kuzingatia mchango wake mkubwa nchini.

Ameitaka Wizara ya Afya kuendelea kuimarisha mfumo wa ufuataliaji wa mwenendo wa magonjwa ya kuambukizwa hasa magonjwa hatarishi ili kupunguza athari zinazoweza kuwapata na kuweka mifumo ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa kifua kikuu kila mwaka.

Dkt. Mpango amewasihiwananchi kujikinga na ugonjwa wa kifua kikuu na kufika hospitalini mara moja pundewaonapo dalili za awali na kuwasihi Watanzania kujijengea utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara.

Wahudumu wa afya wameendelea kusisitizwa kutoa elimu stahiki kwa wananchi na kufuata maadili ya kazi yao.

Kujengwa kwa maabara ya afya ya jamii katika hospitali hiyo utaboresha huduma za tiba nchini pamoja na kupunguza gharama kwa serikali kupeleka sampuli nje ya nchini.

Ujenzi wa maabara hiyo umegharimu shilingi bilioni 12.5.