Huduma za posta kuboreshwa

0
930

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema, serikali itahakikisha huduma za posta nchini zinaendelea kuboreshwa na kukua zaidi.

Amesema hatua hiyo itasaidia kuendana na mapinduzi ya teknolojia duniani na kurahisisha huduma za Posta kuwafikia wananchi wote Barani Afrika.

Waziri Nape ameyasema hayo alipokuwa akihitimisha kilele cha maadhimisho ya miaka 43 ya Umoja wa Posta Afrika, yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.

Amesema Tanzania ina imani na Shirika la Posta Tanzania kupitia huduma linazozitoa kwa kushirikiana na mashirika mengine ya Posta Barani Afrika kuwa itawezesha kuibadili Afrika kuwa ya kidijitali kama ilivyokusudiwa katika Azimio la Umoja wa Afrika.