Mkurugenz wa idara ya huduma kwa wawekezaji kutoka kituo cha uwekezaji nchini TIC Mathew Mnari mesema kufunguliwa tena kwa hoteli yenye hadhi ya kimataifa ya Johari Rotana kutasaidia nchi kunufaika kiuchumi kupitia kodi na ajira kwa watanzania
Mnari ameyaeleza hayo jijini dar es salaam wakati akifungua hoteli hiyo kwa mara nyingine ikiwa ni baada ya kupungua kwa makali ya ugonjwa wa Uviko-19 Duniani
Akizungumza na waandishi wa Habari Mnari amesema wakulima wa mazao ya mbogamboga na nyama ni miongoni mwa watanzania ambao watanufaika na hoteli hiyo kutokana na hoteli hiyo kutumia malighafi za ndani katengeneza chakula
Kwa upande wake Meneja mkuu wa Hoteli hiyo Joerg Potreck amesema kwa sasa hoteli hiyo imeajiri watanzania zaidi ya 200 huku ikitarajiwa kuongeza zaidi idadi ya watumishi wa hoteli hiyo.
Hoteli ya Johari rotana ilisitisha huduma zake nchini mwaka 2020 kutokana na wimbi la ugonjwa wa UVIKO-19.