Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini kukabidhiwa karibuni

0
128

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amekagua na kuweka jiwe la msingi katika hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini, inayojengwa mkoani Mtwara.

Kabla ya kuweka jiwe hilo la msingi, Makamu wa Rais amepokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo,  ambao mpaka sasa umefikia asilimia 97.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amemueleza Dkt. Mpango kuwa pindi itakapokamilika, hospitali hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa elfu moja kwa wakati mmoja.

Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini itatoa huduma katika mikoa ya kanda ya kusini ambayo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi jirani ikiwemo Msumbiji.

Zaidi ya shilingi bilioni 15 zimetumika katika ujenzi wa hospitali hiyo, ambayo inatarajiwa kukabidhiwa kwa Serikali kutoka kwa mkandarasi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) baada ya kipindi cha mwezi mmoja kutoka sasa.