Hospitali ya Nzega yapatiwa Mashine za Oxygen

0
126

Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa taasisi ya Doris Mollel @dorismollelfoundation Doris Mollel, amekabidhi mashine tatu za kufua hewa ya oxygen kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati kwa hospitali ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe @bashehussein ameshukuru kwa mchango huo kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo.

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel @dr_mollel, amepongeza jitihada zinazofanywa na taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuisaidia serikali kupunguza vifo vya watoto wachanga nchini.