Baada ya kukutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango na kuzungumza changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto njiti nchini, Taasisi ya Doris Mollel imekabidhi mashine za kupumulia hewa ya oxygen zenye thamani ya shilingi milioni 12 katika Hospitali ya Wilaya ya Chalinze kwa ajili ya kusaidia watoto njiti wanaozaliwa wilayani humo.
Mashine hizo zilikabidhiwa na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Doris Mollel na kupokelewa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Manedeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete.
Kikwete ameishukuru Taasisi ya Doris Mollel kwa kuwakumbuka wana Chalinze na watoto wachanga wanaozaliwa wilayani humo.