Hoja za Muungano kuendelea kushughulikiwa

0
79

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikishia wananchi kuwa bado inaendelea kushughulikia hoja za Muungano.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mkutano mkuu wa 10 wa CCM mkoani Dodoma, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amesema hoja 14 zimekwishafanyiwa kazi.

Amesema hoja za msingi na zingine nne ambazo zimebaki zitashughulikiwa ndani ya kipindi kifupi kijacho.

Katika hatua nyingine Makamu huyo wa Pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ametaja mafanikio ya serikali hiyo ambayo ni pamoja kufanyika kwa maboresho kwenye sekta ya utalii.

Amesema kwa sasa watalii wameongezewa siku za kukaa Zanzibar kutoka sita hadi kufikia siku nane.

Ameongeza kuwa miaka mitatu iliyobaki ya utekelezaji wa ilani ya CCM, mambo ambayo hayajatekelezwa yatatekelezwa ipasavyo .