Hitimisho Baraza la wafanyakazi TBC

0
76

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Stephen Kagaigai ametoa wito kwa watumishi wa shirika hilo kufanya kazi kwa weledi na nidhamu.

Kagaigai ametoa wito huo alipokuwa akihitimisha kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa TBC leo jijini Dar es Salaam.

Amesema pamoja na kufanya kazi kwa weledi ipo haja ya vijana kupata uzoefu na ujuzi kutoka kwa wale waliowatangulia.

Kikao cha baraza la wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kilichoanza jana kimehitimishwa leo na mwenyekiti huyo.