“Haiwezekani Mheshimiwa Rais na Serikali anayoiongoza watenge fedha wazitoe kwa ajili ya kutatua changamoto za wananchi alafu wale wenye dhamana ya kwenda kutatua wakae mguu upande wasitimize wajibu wao kwa haraka ili kuleta matokeo ya fedha iliyotolewa kwa wananchi.
Hiyo sio sawa na hatutakubaliana nayo, tunachotaka ni kuona kila kilichoahidiwa na kutolewa fedha na Serikali, fedha ile inakwenda kuleta matokeo yakubadilisha maisha ya wananchi na sio maneno na hadithi.”
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Daniel Chongolo