Zaidi ya Hekta 600 za shamba la Taifa la Miti la Sao Hill lililopo wilayani Mufindi mkoani Iringa zimeteketea kwa moto katika kipindi cha wiki moja iliyopita, na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni Tano.
Taarifa hiyo imetolewa kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, -Costantine Kanyasu aliyefika shambani hapo kujionea uharibifu uliotokea.
Meneja Msaidizi wa Shamba hilo lililopo kwenye tarafa ya Tatu, -Siylvester Massawe amemueleza Naibu Waziri Kanyasu kuwa, moto huo umetokea kati ya Oktoba 30 na Novemba Tano mwaka huu.
Kwa mujibu wa Massawe, moto huo katika shamba la Taifa la Miti la Sao Hill umetokana na maandalizi ya mashamba ya Wananchi, ambao wamekua wakiyaandaa kwa kuchoma moto.