Hatuna changamoto ya chakula, tutaendelea kuwa vinara wa uzalishaji

0
113

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema kwa sasa hakuna changamoto ya chakula katika mikoa ya Nyanda za Juu kusini.

Homera ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika sherehe na maonesho ya kimataifa ya wakulima nanenane 2023 zilizofanyika mkoani Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale.

Homera ametaja takwimu za uzalishaji katika mikoa hiyo kuwa katika msimu wa mavuno wa mwaka 2023 mikoa ya nyanda za juu kusini imezalisha jumla ya tani milioni 11.8 za chakula na tani laki 6.69 ya mazao ya biashara ambapo mahitaji ya chakula kwa mikoa hiyo ni tani milioni 2.73 hivyo kufanya mikoa hiyo kuwa na ziada ya chakula ya tani milioni 9.79 na kupelekea mikoa hiyo kuwa kinara wa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Ameongeza kusema kuwa katika kuendelea kuongeza wigo wa uzalishaji Serikali ijielekeze zaidi katika kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji ambayo itawezesha kuongeza uhakika wa uzalishaji kwani itaandaa mazingira mazuri ya kuvutia taasisi za fedha na wadau wengine waliopo katika mnyororo wa thamani wa kuendelea kutoa huduma maalumu ya kuwawezesha wakulima na wafugaji kuzalisha zaidi.