Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Machi 10, 2020 itatoa hukumu ya kesi inayowakabili viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), pamoja na Dkt. Vicent Mashinji.
Katika kesi ya msingi viongozi hao wanatuhumiwa kutenda makosa 13 yakiwemo kufanya kusanyiko na maandamano kinyume na sheria na kutoa maneno ya kichochezi katika siku ya kufunga kampeni ya uchaguzi wa marudio Jimbo la Kinondoni.