Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), Rajab Abdul maarufu Hamronize ametangaza kuanzisha tamasha kubwa la muziki litakalofanyika Uwanja wa Uhuru kuanzia Novemba 28, 2020.
Harmonize amesema tamasha hilo kubwa litafanyika kwa muda wa siku tatu mfululizo na litahusisha wasanii wakubwa wa ndani na nje ya Tanzania.
Mbali na hilo, Harmonize amesema msanii atakayehitaji kutumbuiza kwenye tamasha hilo anatakiwa kutaja kiwango cha bei anachotaka kulipwa pamoja na muda anaotaka kutumbuiza jukwaani.
Tamasha hilo linajulikana kwa jina la Harmo Night Carnival.