Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi amesema viongozi vijana wana jivunia alama ya uongozi aliyoiacha Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kutokana na amna alivyowaandaa vijana kuja kushika nyadhifa mbalimbali za Uongozi
Akizungumza wakati wa hafla ya Maadhimisho ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Hapi amesema Mwalimu alikuwa kiongozi aliyejenga misingi ya uongozi kwa Taifa tangu Uhuru mpaka hivi sasa
Hapi amesema, Mkoa wa Mara utaendelea kuyaenzi mambo yote mazuri yaliyofanywa na baba wa Taifa ili vizazi vinavyokuja viendelee kufaidi kazi nzuri ya Hayati Mwalimu Nyerere
Ameongeza kuwa Mkoa wa Mara, utaendelea kutunza historia ya Mwalimu ili wananchi wa Tanzania waweze kuisoma na kuiendeleza kwa mustakabali wa Tanzania