Halmashauri ya Mji wa Ifakara pamoja na Kilombero kufanyiwa mabadiliko

0
224

Rais John Magufuli amemuelekeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo, kufanya mabadiliko kwa Halmashauri ya Mji wa Ifakara na Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, zilizopo mkoani Morogoro.

Katika maelekezo yake, Rais Magufuli ametaka Halmashauri ya Mji wa Ifakara iongezewe idadi ya Kata kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kilombero na
Makao Makuu yake yawe Ifakara Mjini.

Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Rais Magufuli ameelekeza ibadilishwe jina na iitwe Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, na
Makao Makuu yake yawe Mgeta kama ilivyoamuliwa na Baraza la Madiwani.

Rais Magufuli amewasisitiza viongozi wa Halmashauri wa Mji wa Ifakara na wale wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, kutowayumbisha Wananchi na Watumishi kuhusu utekelezaji wa maelekezo hayo.

Amemuagiza Waziri Jafo kusimamia utekelezaji wa maelekezo hayo kwa mujibu wa sheria.