HALI YA KISIASA: HATUA ZA RAIS SAMIA KATIKA KUIMARISHA DEMOKRASIA

0
1323

NCHI IWE NA AMANI

“Kwanza nchi iwe na amani sio tu amani ya kutokupigana ni amani za moyoni mwetu, kwanza ukimjengea mtu amani ya moyo wake anakuwa huru kuendesha mambo yake”.

UHURU NAO ULINDWE

“Lakini na uhuru nao ulindwe, ulindwe wa huyu mwenyewe na ajue mwisho wa uhuru wangu unaanza uhuru wa mtu mwingine, asiwe huru kiasi cha kumuudhi mwingine aaah twende vizuri”

KUWATOA WATU HOFU

“Kuwatoa watu hofu kwenye kuishi na mimi, siku zote nasema hii ni nchi yetu sote, mtu wa chama chochote asie chama wa dini yoyote asie dini wa kabila lolote asie na kabila kama mimi, hii ni nchi yetu sote kwa hiyo kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha hii nchi inakwenda vizuri.”

LAZIMA TUZUNGUMZE, LAZIMA TUJENGE MAZINGIRA MAZURI

“Kuendesha nchi haimtegemei mtu mmoja, uendeshaji wa nchi ni makubaliano, maridhiano, mkubaliane mnaendeshaje nchi na si kuvutana maana mnapovutana mara zote haijaonesha matokeo chanya, lakini mnapozungumza wewe ukasema lako mwenzako akasema lake mnaona tumekosea wapi na mnakaa kurekebisha mlipokosea hali inakwenda vizuri.”

KUAMINIANA

“Kuaminiana kwanza waone unachokisema ndio unachokifanya kama kiongozi wao , na kama ukishindwa umejaribu kufanya lakini hakikuwa jitihada zinaendelea.”


KUFUATA SHERIA

“Tunakubaliana tuna kwendaje kama nchi, twende hivi sheria ziheshimiwe, asiye heshimu sheria hapa sasa tutakamatana lakini kwanza tumezungumza, tumekubaliana twende hivi”

Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo katika mahojiano maalum na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt.Ayub Rioba Chacha, mahojiano yanayoangazia mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya sita madarakani.