Watu mbalimbali wamefika katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera, inapofanyika shughuli ya kuaga miili ya watu 19 waliofariki dunia katika ajali ya ndege hapo jana.
Shughuli ya kuaga miili ya watu hao inaongozwa na waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Katika ajeli hiyo ya ndege mali ya Shirika la Ndege la Precision Air, watu wengine 26 waliokolewa wakiwa hai.