Ada kifato cha 5 na 6 kufutwa

0
169

Wizara ya Fedha Imependekeza kufutwa kwa ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita.

Akiwasilisha bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kwa hatua hiyo elimu bila ada itakua kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita.

Amesema kwa sasa wanafunzi wa kidato cha tano ni takribani elfu 90 na kidato cha sita ni takribani elfu 56 ambao wote watanufaika na hatiua hiyo.

Dkt. Nchemba amesema kufutwa kwa ada kidato cha tano na kidato cha sita ni maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan , engo likiwa ni kupunguza gharama kwa wazazii na walezi wa wanafunzi hao.