HABARI PICHA KUTOKA – LINDI

0
235

Rais John Magufuli akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka huu Mzee Mkongea Ally, wakati wa sherehe za kilele cha mbio za Mwenge, wiki ya Vijana Kitaifa na kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika uwanja wa michezo wa Ilulu mjini Lindi.

Wabunge wa mkoa wa Lindi na Viongozi wengine, wakiserebuka na Msanii Rajabu Abdul Kahali maarufu kama Harmonize ama Konde Boy, kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge, maadhimisho ya wiki ya Vijana Kitaifa na kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, sherehe zilizoongozwa na Rais John Magufuli katika uwanja wa michezo wa Ilulu mjini Lindi.

Rais John Magufuli akiwa jukwaa kuu na viongozi wengine wa Kitaifa, kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, maadhimisho ya wiki ya Vijana Kitaifa na Kumbukumbu ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, sherehe alizoziongoza katika uwanja wa michezo wa Ilulu mjini Lindi.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengine wakiserebuka na Msanii Rajabu Abdul Kahali maarufu kama Harmonize ama Konde Boy kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, maadhimisho ya wiki ya Vijana Kitaifa na Kumbukumbu ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, sherehe zilizoongozwa na Rais John Magufuli katika uwanja wa michezo wa Ilulu mjini Lindi.