Jeshi la polisi mkoani Pwani, linamshikilia mkazi mmoja wa jijini Dar es salaam baada ya kukamatwa akisafirisha gunia Tisa za bangi kutoka mkoani Morogoro kwenda jijini Dar es salaam.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa ameiambia TBC kuwa, mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari wa doria kwenye eneo la Sheli Maili Moja mjini Kibaha akiwa amepakiza gunia hizo za bangi katika gari ndogo aina ya Prado lenye namba za usajili T 855CYP.
Kamanda Nyigesa
amesema kuwa katika gari hiyo, mtuhumiwa huyo Mkazi wa Mwananyamala alikuwa na watu wengine watatu ambao baada ya kusimamishwa na polisi walitoroka na sasa polisi inaendelea kuwatafuta.
Mtuhumiwa huyo kwa sasa anashikiliwa katika kituo cha polisi Kibaha Mjini, na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.