Mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigela leo amewaapisha wakuu wa wilaya wapya watatu walioteuliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo.
Miongoni mwa wakuu hao wapya wa wilaya waliopishwa ni Grace Kingalame, mkuu wa wilaya ya
Nyang’hwale ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa mtumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Wakuu wengine wa wilaya walioapishwa kwa mkoa wa Geita ni Colnel Magembe, mkuu wa wilaya ya Geita na Deusdedith Katwale, mkuu wa wilaya ya Chato.
Wakuu hao wa wilaya wapya wa wilaya za mkoa wa Geita mara baada ya kuapishwa na mkuu wa mkoa huo pia wamekula kiapo cha ahadi na uadilifu.