‘Google Photos’ kuanza kulipiwa

0
658

Kampuni maarufu duniani inayojishulisha na masuala ya TEHAMA ‘Google’ itaanza kulipisha watumiaji wake wa mtandao wao wa kuhifadhi picha mtandaoni (Google Photos) ifikapo Juni 2021.

Mtandao huo ambao upo wazi kwa kila mwenye akaunti ya Google, umekuwa ukitoa huduma ya uhifadhi picha bure huku ukiweza kuhifadhi picha kwa kiasi unachoweza.

Kama ilivyo kwa biashara mbalimbali kubadli mifumo yao ufanyaji kazi ama kuongeza gharama, Google nao hawakuwa mbali. Afueni ni kwamba, kama hukuwahi kutumia Google Photos bado unaweza kuhifadhi picha zako kwa kipindi hiki na kwa wale ambao tayari wanmehifadhi picha zao hazitoathiriwa na mfumo huo mpya. Ila chochote utachoongeza kuanzia Juni 2021 utalazimika kulipia.

Ikumbukwe kuwa Google hutoa Gigabytes 15 (15GB) kwa kila mtu mara ufunguapo akaunti na hii ni mbali na huduma ya bila kikomo (unlimited) ya kuhifadhi picha.

Mabadiliko mengine yanayotarajiwa kufanyika ni pamoja na maboresho ya Google sheets, Docs pamoja na Google slides kujumuishwa kwenye nafasi hiyo ya 15GB za bure.