GGM yachangia moja ya tatu ya makusanyo Geita Mji

0
613

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Geita, Costantine Morandi amesema, moja ya tatu ya mapato katika halmashauri yake yanatokana na kodi na tozo mbalimbali zitokanazo na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM).

Akitoa taarifa ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya kusaidia jamii kati ya mkoa wa Geita na GGM, Morandi amesema kwa kiasi kikubwa mkoa wa Geita umekuza uchumi wake kutokana na uwepo wa mgodi huo.

Ameongeza kuwa fedha zinazokusanywa na zile za kusaidia jamii ya halmashauri hiyo kutoka GGM zimechagiza kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika wilaya hiyo.

Morandi amesema, miradi ya maji, afya, elimu na miundombinu itapata fedha na kuharakisha ujenzi wake, ili iweze kuwasaidia wanajamii wa Geita.