Gesi asilia yafanikisha upatikanaji wa nishati nchini

0
142

Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Khalfan Khalfan amesema Serikal imepiga hatua kubwa katika kufanikisha upatikanaji wa nishati majumbani kupitia shirika la umeme nchini (TANESCO) ambalo amesema asilimia 60 ya nishati yake inatokana na gesi asilia inayozalishwa hapa nchini.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika viwanja vya Sabasaba yanapoendela maonesho ya 46 ya biashara kimataifa ya Dar es Salaam.

Sambamba na hilo ameeleza faida zitokazotokana na uwekezaji kwenye mradi wa kuzalisha gesi asilia kuwa kimiminika LNG, ambapo amesema ujenzi wa mradi huo utatoa fursa za ajira takribani elfu 10 kwa wananchi na utaongeza pato la taifa na kusaidia kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa nishati nchini.

Amesema kwa sasa mtumiaji mkubwa wa gesi nchini ni shirika la umeme TANESCO ambapo linatumia takribani asilimia 60 ya gesi inayopatikana nchini kwaajili ya kuzalisha umeme hivyo amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika mikakati yake ya uwekezaji kwani bila kuwapa wawekezaji miradi hiyo isingekuwepo.