Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga, Safia Jongo amepiga marufuku gari zisizokaguliwa kubeba wanafunzi pindi shule zitakapofunguliwa na kusisitiza kuwa yeyote atakayekiuka agizo hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Kamanda Jongo ametoa kauli hiyo wakati wa zoezi maalum la ukaguzi wa gari zinazobeba wanafunzi mkoani Tanga, uliofanyika kwenye makao makuu ya trafiki Mabawa jijini Tanga.
Amesema wakati umefika kwa wazazi na walezi kushirikiana katika usimamizi wa zoezi hilo, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi wanapoona gari za shule zimebeba wanafunzi kupita uwezo.