Gabriel : Mkashughulikie changamoto za Wananchi

0
146

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel amewaagiza Wakuu wa wilaya aliowaapisha hii leo kufanya kazi kwa weledi na kwenda kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wananchi ikiwa mi pamoja na migogoro ya ardhi na mirathi.

Pia amewataka kwenda kusimamia uboreshwaji wa miundombinu ili isaidie katika kukuza uchumi kwenye maeneo yao, na kuepuka vitendo vya rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Wakuu wapya wa wilaya za mkoa wa Mwanza walioapishwa hii leo ni wa Nyamagana, Ilemala na Kwimba.