Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Tano Mwera amesema ipo haja ya kuwaelimisha wenyeji wa Kalambo kuhusu uwepo wa samaki wa mapambo katika ziwa Tanganyika.
Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo wakati akizungumza na waandaji wa vipindi vya Utalii vinavyorushwa na TBC kupitia Chaneli yake ya Tanzania Safari.
Mwera ameeleza kuwa watu wengi hawana ufahamu kama ziwa Tanganyika linapatikana pia mkoani Rukwa katika Wilaya ya Kalambo na kudhani lipo Mkoani Kigoma pekee
Amesisitiza kuwa uwepo wa samaki wa mapambo katika ziwa Tanganyika ni moja kivutio ambacho wananchi wa wilaya hiyo wanapaswa kufahamu kwa muktadha wa kutembea na kujionea.
Vivutio vingine vya kitalii vinavyopatikana Wilayani Kalambo ni pamoja na Bwawa la asili Sundu, Ngome ya Bismarck, Chemchem ya majimoto Kizombwe na Majengo ya kale na Ziwa Tanganyika.